HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Katibu katika wizara ya Kilimo ashtakiwa kwa sakata ya NCPB

Katibu katika wizara ya kilimo Dkt Richard Lesiyampe pamoja na aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa bodi ya nafaka na mazao NCPB Newton Terer wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3 pesa taslimu kila mmoja baada ya kushtakiwa kuhusu sakata ya mahindi ya shilingi bilioni 11.
Maafisa wa kukabiliana na ufisadi, EACC waliwakamata baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Hajji kuagiza wakamatwe kwa madai ya kuhusika katika ununuzi wa mahindi kwa njia isiyokubalika kisheria.
Washukiwa wengine wanane kati ya 16  walio katika orodha ya Noordin Haji wanazidi kusakwa.

Show More

Related Articles