HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Yamwachilia Katibu Katika Wizara Ya Kilimo Lesiyampe Na Dhamana Ya Shilingi Milioni 3

Hakimu wa mahakama ya  kupambana  na ufisadi Francis Kombo amewaachilia katibu wa kudumu katika  wizara ya kilimo Richard Lesiyampe ,na washukiwa wawili wengine kwa dhamana ya shilingi milioni 3 kila mmoja  kwa makosa saba kuhusiana na kupotea kwa mamilioni ya pesa katika bodi ya kitaifa ya nafakaNCPB.

Mahakama pia imewapa njia mbadala ya kulipa dhamana binafsi ya shilingi milioni 6 na mdhamini wa kiasi sawa.

Watatu hao pia wametakiwa kupeana paspoti zao na kutowasiliana na mashahidi.

Wote wanakabiliwa na mashtaka ya kuzidisha bajeti  wakati wa kununua magunia milioni mbili ya mahindi katika mwaka wa kifedha wa 2017/2018.

Show More

Related Articles