People Daily

Serikali Ya Kenya Na Ile Ya Uingereza Ya Saini Mkataba Wa Ushirikiano.

Serikali ya Uingereza imetia saini mkataba  ushirikiano  na  serikali ya kenya  kwenye vita dhidi ya ufisadi vinavyoendelea nchini.

Akiongea katika ikulu ya Rais jijini Nairobi waziri mkuu wa uingereza Theresa May anasema atahakikisha fedha za umma zilizoibwa na kufichwa katika mabenki nchini uingereza zinarejeshwa nchini.

May amesema pesa hizo zitatumika kufadhili miradi ya maendeleo hasa katika sekta za afya , usalama na elimu.

Rais Uhuru Kenyatta kwa upande wake ameeleza kuridhia hatua hiyo akisema itasaidia kufanikisha vita dhidi ya ufisadi vinavyoendelea nchini.

Kando na hayo waziri  May amesema pia serikali yake itasaidia kenya kwenye vita dhidi ya ugaidi ili kuimarisha usalama katika kanda ya afrika mashariki.

 

Show More

Related Articles