HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Kuu Yasimamisha Kwa Muda Mashataka Dhidi Ya Naibu Jaji Mkuu.

Mahakama kuu kupitia jaji Chacha Mwita imesimamisha kwa muda mashtaka dhidi ya naibu jaji mkuu Philomena Mwilu hadi tarehe 9 ya  mwezi oktoba.

Hii ni baada ya mawakili wanaomwakilisha Mwilu kuelekea katika mahakama hiyo na kutafuta agizo la kutaka mashtaka dhidi yake yanayoendelezwa na mahakama ya hakimu yasimamishwe kwa muda

Awali wakili  wa Mwilu James Orengo aliiambia mahakama kwamba mashtaka ambayo anapaswa kujibu mteja wake ni mashtaka ambayo yamejengwa kwa msingi wa kisiasa.

Show More

Related Articles