HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanajeshi 5 Wapoteza Maisha Yao Baada Ya Gari lao Kukanyaga Kilipuzi.

Wanajeshi 5 wa KDF wamepoteza maisha yao huku wengine 10 wakipata majeraha baada ya gari waliokua wakisafiria  kukanyaga kilipuzi katika barabara ya Kiunga-sankuri kaunti ya lamu.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari msemaji mkuu wa KDF Kanali Paul Njuguna amethibitisha kisa  hicho akisema tukio hilo limetokea mwendo wa saa 2 asubuhi pale ambapo maafisa hao walikua katika shughuli za kuteka maji na kuwasambazia wenyeji wa sehemu hiyo.

Amewashukuru wenyeji kwa kuwasaidia maafisa waliojeruhiwa na pia kuwarai watoe msaada wowote utakaofanikisha juhudi za serikali kwenye vita dhidi ya ugaidi.

Show More

Related Articles