HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaopania Kuwekeza Katika Kaunti Ya Taita Taveta Waombwa Kuzingatia Sheria.

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta kupitia kwa wizara ya ardhi imesema haijatoa idhini ya kujengwa chuo kikuu  cha Diaspora mjini Mwatate.

Kulingana na katibu wa wizara ya ardhi, mazingira na raslimali kaunti hiyo Claris Mnyambo bado haijaafikiwa wawekezaji kuanzisha shughuli zozote za ujenzi kwani bado serikali inaendeleza vikao vya kuhamasisha na kupata maoni kutoka kwa wakaazi wa eneo la hilo.

Haya yanajiri miezi michache baada ya gavana Granton Samboja kusema wawekezaji wote wanaozuru kaunti hiyo na wanaopania kuwekeza katika  kaunti hiyo sharti wafuate sheria.

Show More

Related Articles