HabariPilipili FmPilipili FM News

Hudma Katika Hospitali Za Umma Huenda Zikatatizika Kutokana Na Deni La Dawa.

 

Huenda hospitali za umma zikalazimika kusimamisha hudumu muhimu wakati huu ambapo serikali za kaunti zinadaiwa deni kubwa na mamlaka za kusambaza dawa nchini.

Hii ni baada ya kubainika kuwa mamlaka hizo ikiwemo KEMSA inadai serikali hizo takriban shilingi bilioni 1.4.

Inaarifiwa kuwa hospitali hizo hazijailipa KEMSA jumla ya shilingi bilioni 1.2, hatua ambayo huenda ikasimamisha KEMSA kusambaza dawa ambapo wakenya wengi huenda wakaathirika na ukosefu wa dawa.

Kufikia tarehe 17 ya mwezi huu, hospitali za umma kaunti ya Nairobi zilikuwa zinadaiwa kiwangi cha juu cha deni la shilingi milioni 234 ikilimganishwa na kaunti nyingine.

 

 

 

Show More

Related Articles