HabariMilele FmSwahili

Muungano wa wenye matatu kuongeza nauli kuanzia jumamosi hii

Kuanzia jumamosi hii, wakenya wataanza kulipia nauli iliyo ongezwa. Muungano wa wenye matatu umeamua kuongeza nauli hiyo baada ya serikali kuanza kutoza ushuru wa asilimia 16 bidhaa za petroli. Mwenyekiti wa muungano huo Simon Kimutai anasema nauli ya chini kwa magari ya uchukuzi kulipisha itakuwa shilingi 30. Kadhalika anasema mashauriano yameanza kati yao na wadau mbali mbali katika sekta hii kuhakikisha nauli zinawiana na mwendo wa safari ikizingatiwa bei ya mafuta maeneo mbali mbali nchini.

Show More

Related Articles