HabariMilele FmSwahili

Ali Korane apuuza madai ya kukamatwa na polisi mapema leo.

Gavana wa garissa Ali Korane amepuuza madai kwamba alikamatwa na polisi mapema leo akihusishwa na kisa cha kufwatuliwa risasi aliyekuwa waziri wa fedha kaunti yake Idris Adan Muktar. Katika ujumbe alioupachika katika mtandao wake wa Twitter, Korane badala yake anasema alijisalimisha mwenyewe kwa polisi na kwamba tayari ameandikisha  taarifa kwa idara ya upelelezi kuhusu kisa hicho. Juma lililopita genge la majambazi watatu lilimfumania Mukhtar na kumpiga risasi kichwani na kutoweka bila kumwibia chochote.  Chanzo cha uvamizi huo hakijabainika.

Show More

Related Articles