HabariPilipili FmPilipili FM News

Viongozi Wa Dini Kaunti Ya Kwale Waomba Serikali Kupiga Marufuku Mikutano Ya Siku Ya Ijumaa

Mwenyekiti  wa kamati inayosimamia masuala ya bajeti kaunti ya Kwale na aliyepia  kiongozi  wa dini ya jamii ya waislam  Sheikh Kassim Zani ametoa changamoto kwa viongozi  kupiga marufuku mikutano   ya siku ya ijumaa  akisema kuwa siku hiyo imetengwa kwa jamii ya waislam kufanya ibada zao.

Sheikh Zani anadai kwamba shughuli za siku ya ijumaa zinakiuka misingi ya dini ya kiislam hivyo kusema kwamba  ataanzisha mchakato mzima  wa  kueneza injili kwa jamii ya  waislam kutohudhuria mikutano ya siku ya ijumaa.

Hii ni  baada ya  mkao wa  kutoa  maoni mapendekezo ya miradi ya maendeleo  katika mwaka  huu wa fedha  2018/2019  kaunti  ya  kwale  kufanyika  siku  ya  ijumaa  juma lililopita.

Show More

Related Articles