HabariPilipili FmPilipili FM News

Miili Ya Watu Wawili Waliozama Baharini Hapo Jana Yapatikana.

Hatimaye miili ya watu wawili waliozama kwenye Kivuko cha Kwa Jomvu Misheni hapa Mombasa baada ya mashua waliokuwa wakivukia kuzidiwa na mawimbi makali ya bahari imepatikana.

Mwili wa mtoto mmoja uliokuwa ukitafutwa baada ya kuzama ulipatakina jana usiku huku mwili wa mwanamke ukipatikana leo.

Wawili hao walikuwa miongoni mwa watu 12 waliokuwa wamezama baada ya dau walilokuwa wameabiri kupinduka.

Walikuwa wanatoka maeneo ya MAUNGUJA kuelekea jomvu misheni kabla ya ajali hiyo kutokea.

Watu 9 kati ya 12 waliokuwa wameabiri dau hilo waliokolewa salama hapo jana.

Show More

Related Articles