HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Uchunguzi waanza kuhusu matumizi ya Ksh 1.7B za mashindano ya chipukizi

Katibu katika wizara ya michezo Peter Kaberia alikuwa na wakati mgumu kuelezea ni vipi serikali ilipoteza jumla ya shillingi billion 1 nukta 7 katika maandalizi ya michezo ya kuwania ubingwa wa dunia ambayo Kenya iliandaa mwezi Julai mwaka jana jinsi ilivyonukuliwa katika ripoti ya mhasibu mkuu wa serikali Edward Ouko.

Kaberia, ambaye alifika mbele ya kamati ya bunge ya uhasibu alishindwa kuelezea ni vipi wizara hiyo iliruhusu baadhi ya wanachama katika kamati andalizi kuidhinisha matumizi ya jumla ya shilingi milioni 350 kwa huduma za usafiri bila kumhusisha mkuu wa uagizaji wa kamati andalizi wakati huo Duncan Ashume.

Show More

Related Articles