HabariPilipili FmPilipili FM News

Watatu Hawajulikani waliko Baada ya Boti Waliokua Wakisafiria Kuzama Baharini.

Watu 3 hawajulikani waliko baada ya boti walilokuwa wakisafiria kuzama baharini eneo la Jomvu Mishen.

Akithibitisha tukio hilo  afisa wa majanga ya dharura eneo la miritini Bakari Ali Nyundo,anasema boti hiyo ilikuwa na watu 12 wakati wa mkasa huo uliotokea jana jioni huku  Watu 8 wakiokolewa  na kikimbizwa  hospitalini kupokea matibabu, huku Shughuli za kuwatafuta Watu 3 akiwemo mama mmoja na watoto 2 wanaoaminika kuzama baharini zikiendelea.

Afisa huyo ametoa wito kwa  jamii kuwa wangalifu na pia wenye vyombo vya baharini kuzingatia usalama wao na abiria ili kuepuka maafa zaidi, hasa wakati huu ambapo kunashuhudiwa mawimbi makali baharini.

 

Show More

Related Articles