HabariPilipili FmPilipili FM News

Walimu Watishia Kugoma Kuanzia Mwezi Ujao.

Huku shule zikifunguliwa rasmi hii leo,wasiwasi umetanda kuhusiana na masomo muhula huu wa tatu baada ya chama cha walimu KNUT kutishia kugoma tarehe 1 mwezi ujao.

Katibu mkuu wa KNUT Willson Sossion anasema mkutano waliofanya na muajiri wao TSC kuhusiana na matakwa yao haukuzaa matunda hivyo hawana budi ili kushiriki mgomo huo.

KNUT inataka TSC ishughulikie masuala kadhaa ikiwemo uhamisho wa walimu.

Haya yanajiri huo wenzao wa KUPPET na KEPSHA wakitofautiana na hatua hiyo.

Show More

Related Articles