HabariPilipili FmPilipili FM News

Nauli Ya Matatu Yatarajiwa Kupanda Kutokana Na Ongezeko La Bei Ya Mafta.

Huenda abiria wanaotumia usafiri wa umma wakalazimika kulipa nauli ya juu zaidi baada ya wenye matatu kunuia kupatandisha nauli kutokana na hatua ya serikali kuongeza ushuru wa mafuta kwa asilimia 16.

Kulingana na mshirikishi wa chama cha wenye matatu ukanda wa pwani  Salim Mbarak, matatu zinazohudumu katika mji wa Mombasa zitaongeza nauli kwa shilingi 10 huku zile zinasosafiri nje ya mji zikiongeza nauli kwa shilingi 50 kuanzia siku ya Jumamosi.

Mbarak amesema hatua hiyo huenda ikabadilika iwapo serikali itaondoa nyongeza ya ushuru wa asilimia wa mafuta.

Show More

Related Articles