HabariMilele FmSwahili

Makamishna 3 waliojizulu warejea kazini IEBC

Makamishna 3 waliotangaza kujiuzulu miezi 4 iliyopita sasa wamerejea kazini rasmi leo. Tatu hao Consolata Nkatha, Margaret Mwachanya and Paul Kurgat wanadai kurejelea nafasi zao baada ya rais Kenyatta kukosa  kutangaza nafasi zao kuwa wazi. Hii ni licha ya mwenyekiti Wafula Chebukhati kudhibitisha kuwa makamishna hao walidhibitisha katika hati kiapo kujiuzulu. Yakijiri hayo baadhi ya viongozi wa  ODM wamejiunga na wanaopinga kurejea kazini makamishna watatu wa IEBC waliojiuzulu miezi minne iliyopita. Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi na mwenzake wa Gem Elisha Odhiambo wameshikilia kuwa kurejea kazi kwa tatu hao ni kinyume na sheria. Wameitaka IEBC kuharakisha mchakato wa kuwateua makamishna wapya. Kauli sawa ikitolewa na gavana wa Siaya Cornel Rasanga.

Show More

Related Articles