HabariK24 TvSwahiliVideos

Gavana wa Mombasa Hassan Joho afanya mkao na rais mstaafu, Kabarak

Joho

Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho mapema Jumamosi alikutana na rais mstaafu Daniel Arap Moi pale Joho alipomtembelea mzee Moi nyumbani kwake eneo la Kabarak kaunti ya Nakuru.

Joho alipokelewa na Seneta wa Baringo Gedion Moi kabla ya wawili hao kufanya kikao faraghani kwa takriban saa moja.

Taarifa kutoka kwa afisi ya Moi zimearifu wawili hao walijadili masuala muhimu ya kitaifa, yaliyohusisha siasa na uwiyano wa kitaifa.

 

Show More

Related Articles