HabariK24 TvSwahiliVideos

Zimwi La ufisadi : Mwakilishi wa wadi ya Parkland Jahendra Malde  akamatwa

Ufisadi

Maafisa wa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini[EACC] wamemkamata mwakilishi wa wadi ya Parklands Jahendra Malde.

Inadaiwa kuwa Jahendra alikuwa anaitisha hongo ya Milioni 5.7 kutoka kwa mmiliki wa hotel ya Concord katika eneo la Westlands hapa jijini Nairobi huku akimuahidi kwamba hoteli yake haitabomolewa na serikali ya kaunti ya Nairobi. Malde atasalia rumande hadi siku ya Jumatatu atakapofikishwa mahakamani.

 

Show More

Related Articles