HabariPilipili FmPilipili FM News

Tume Ya Kuajiri Walimu Ya Kubaliana Na KNUT Kuunda Kamati Itakayo Angazia Lalama Za Walimu

Wakuu wa chama cha walimu nchini KNUT wameafikiana na tume ya kuajiri walimu nchini TSC kubuni kamati ya watu sita, kuangazia lalama za walimu ikiwemo suala tata la uhamisho.

Hayo yameafikiwa katika mkutano uliowaleta pamoja maafisa kutoka pande zote mbili, kujadiliana kufuatia agizo la rais kwamba baadhi ya sera za walimu ziangaziwe upya.

Mwenyekiti wa chama cha walimu nchini KNUT Wycliff Omucheyi anasema kamati hiyo, itafanyia tathmini masuala tata kabla ya tarehe 30 pale watakutana tena kujadiliana kuhusu mwelekeo utakaochukuliwa.

Show More

Related Articles