People Daily

Wakenya Wanaofanya Kazi Nchi Marekani Watajwa Kuwa Na Bidii Zaidi.

Wahamiaji kutoka nchini Kenya wanaofanya kazi nchini Marekani wameorodheshwa katika nafasi ya tatu kati ya wahamiaji wa kigeni wanaofanya kazi kwa bidii zaidi nchini humo.

Wafanyakazi wa Kenya walipata alama 73.4 kuchukua nafasi ya tatu miongoni mwa wafanyakazi wenye ujuzi zaidi na bidii nchini Marekani kwa mujibu wa ripoti ya Bloombeerg ya mwaka 2018

Utafiti huo unawaweka raia wa Ghaana katika nafasi ya kwanza na wale wa Bulgeria kwenye nafasi ya pili wakiwa na asilimia 75.2 na 74.2 mtawalia.

Nchi zingine za Afrika zinazotajwa katika orodha ya kumi bora ni Ethiopia nafasi ya nne, Misri nafasi ya tano, Nigeria nafasi ya nane na Liberia nafasi ya tisa.

Show More

Related Articles