HabariPilipili FmPilipili FM News

Hati Miliki Ya Kipande Cha Ardhi Ya Kibarani Yaregeshwa Katika Tume Ya Ardhi Nchini NLC.

Kampuni ya General Tires Mombasa inayomiliki kipande cha ardhi katika eneo la Kibarani imesalimisha hati miliki ya ardhi yake kwa tume ya ardhi nchini NLC.

Akram Mohammed aliyejisalimisha kama rafiki wa mmiliki wa kipande hicho cha ardhi amesema kampuni ya General Tires imeamua kufanya hivyo baada ya kusikia serikali initaka eneo hilo kwa matumizi ya umma.

Hata hivyo hadi kufikia uamuzi huo kampuni ya General tires haikuwa imewekeza chochote kwenye kipande hicho cha ardha na hata licha kwamba kampuni hiyo imekuwa ikilipa  ada zake kila mwezi kwa serikali,imesema haitaki kulipwa chochote.

Kwa upande wake tume ya ardhi nchini ikiongozwa na naibu mwenyekiti wake Abigaeile Bagaye imepongeza hatua hiyo na kutoa wito kwa wakenya wengine kuiga mfano huu.

 

Show More

Related Articles