HabariMilele FmSwahili

NTSA yafutilia mbali leseni za kuhudumu za mashirika 3 za usafiri

Mamlaka ya usalama barabarani NTSA imefutilia mbali leseni za  kuhudumu za  mashirika 3 ya usafiri kwa kukiuka sheria.Katika ujumbe NTSA inasema mashirika ya Kidatho , Silker Agencies na lile Giwa hayana kibali cha kuendesha shughuli za usafiri.NTSA inasema  imechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mashirika hayo yamekwenda kinyume na sheria za usafiri za mwaka wa 2014.Mkurugenzi wa NTSA Francis Mejja amewataka wasafiri  kujitenga na magari hayo.

Show More

Related Articles