HabariMilele FmSwahili

Wito wazidi kutolewa kwa wakenya kukumbatia masomo ya kiufundi

Mbunge wa Mbeere Kusini kaunti ya Embu Geofrey Kingangi ametoa wito kwa wakazi eneo hilo kukumbatia  masomo ya kiufundi. Kingangi anasema serikali imeweka mikakati ya kufadhili masomo ya wanafunzi wanaojiungha na vyuo hivyo wakazi hawapaswi kupuuza taasisi hizo. Amewataka wazazi kuwaruhusu wanao wasioweza kujiunga na vyuo vikuu kuhudhuria masomo katika vyuo hivyo ili kukuza vipaji na ujuzi  pia ameapa kuinua viwango vya masomo Mbeere Kusini eneo hilo likishikilia mkia katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kwa miaka 5 iliyopita.

Show More

Related Articles