HabariMilele FmSwahili

Ruto kufanya ziara Trans Nzoia leo kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo

Naibu rais William Ruto leo anatarajiwa kufanya ziara katika kaunti ya Trans Nzoia kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo. Naibu rais atazindua ukarabati wa bara bara ya Lessos-Namanjalala-Maili 11. Pia atazindua bara bara nyingine eneo kwanza ya Maili kumi na moja kuelekea Kolongolo hadi Chepchoina. Baadaye Ruto ataelekea Endebess kufungua rasmi afisi za CDF na kituo cha kukusanya mbengu cha ADC na  mradi wa uekaji taa za  bara barani. Naibu rais atahutubia mikutano kadhaa ya hadhara kwenye ziara hiyo. Wakati uo huo Ruto ameendelea kuwazima wanaompaka tope kwa kumhusisha na madai ya ufisadi akisema njama yao haitafaulu. Akiongea huko Kisii, amesema ataendelea kuchapa kazi ili kuimarisha zaidi rekodi yake ya maendeleo.

Show More

Related Articles