HabariMilele FmSwahili

Afueni kwa wakulima Trans Nzoia serikali ikitoa shilingi bilioni 1.4 kuwalipa

Ni afueni kwa wakulima wa mahindi kanda ya Northrift baada ya serikali kutoa shilingi bilioni moja nukta nne kama malipo kwa waliowasilisha mahindi kwa bodi ya mazao  na nafaka mwaka jana .  Mwenyekiti wa  hifadhi ya kitaifa ya chakula Noah Wekesa anasema  wakulima watalipwa kuazia juma hili. Pia amesema kiasi kilichosalia cha shilingi bilioni mbili unusu kitatolewa kabla ya msimu huu wa mavuno.Naye waziri wa ugatuzi Eugine Wamalwa wakulima  wote watalipwa pindi wanapowasilisha mazao yao  kwa maghala ya NCPB ili kuzuia kucheleweshwa malipo yao.

Show More

Related Articles