HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Bobi Wine aachiliwa na jeshi kabla ya kukamatwa na polisi

Kufuatia malalamishi kutoka kwa mataifa ya kigeni na mashirika ya kutetea haki za kibinadam kufutia kukamatwa kwa mbunge wa Chadondo Mashariki  Robert Kyagulanyi almarufu Bobi Wine, mbunge huyo aliachiliwa leo na jeshi kabla ya kukamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa mashtaka kadhaa likiwemo shtaka la uhaini kwa kimombo treason.
Haya yanajiri huku chama cha mawakili nchini LSK pamoja na watetezi wa haki za kibinadamu wakiandamana jijini Nairobi kushinikiza serikali ya Yoweri Kaguta Museveni kokoma kukandamiza haki za viongozi nchini mwake.

Show More

Related Articles