HabariPilipili FmPilipili FM News

Kizazaa Cha Shuhudiwa Katika Ofisi Za Tume Ya Adhi, Mombasa.

Vurugu zimeshuhudiwa katika ofisi za tume ya ardhi kaunti ya Mombasa baada ya watetezi wa haki za binaadam kutoka  kaunti hiyo kuvamia ofisi hizo na kuwataka maafisa wa tume hiyo wanaohudumu katika ofisi hizo kujiuzulu.

Wakizungumza kwa ghadhabu watetezi hao kutoka shirika la Haki Afrika,Muhuri na mashirika mengine wameitaka tume hiyo kuhakikisha ardhi zote za umma zilizonyakuliwa na mabwenyenye kinyume cha sharia zinarudishwa mikononi mwa umma.

Wamesema takriban vipande vya ardhi 600 vinavyoishi zaidi ya watu elfu mbili vinamilikiwa kinyume cha sharia huku wakitaka majengo yalio kwenye vipande hivyo kubomolewa haraka iwezekanavyo.

Maeneo waliyoyatajwa kuwa na vipande hivyo vya ardhi ni Kizingo,Mama ngina,Marikiti,Kingorani miongoni mwa maeneo mengine.

Show More

Related Articles