HabariPilipili FmPilipili FM News

Naibu Rais William Ruto Awajibu Wapinzani Wake.

Naibu rais William Ruto anasema hatobabaishwa na siasa zinazoendelezwa na wapinzani wake.

Amesema yeye kwa ushirikiano na rais Uhuru Kenyatta wako imara ambapo ajenda yao kuu ni kuwahudumia wakenya na kuhakikisha serikali inaafikia mipango yake ya maendeleo.

Aidha amesema ako tayari kwa mashindano na wanaompinga, akisema mashindano ya uhakika ni yale yanayoegemea kubadilisha maisha ya wakenya.

Ruto ameongea haya mapema leo wakati wa mkutano wa kiamsha kinywa na gavana wa kirinyaga Anne Waiguru katika kikao kilichojumuisha wajumbe 33 kutoka eneo la kati mwa nchi.

Show More

Related Articles