HabariMilele FmSwahili

Hafla ya ukumbusho wa aliyekuwa makamu wa rais Kijana Wamalwa yafanyika Saboat

Suala la umoja wa jamii ya Magharibi ndilo litatawala hafla ya ukumbusho wa aliyekuwa makamu wa rais Kijana Wamalwa inayofanyika nyumbani kwake huko Saboat kaunti ya Trans Nzoia.Viongozi wanaohudhuria wakiwemo nduguye marehemu ambaye ni waziri Eugine Wamalwa wanasema wanataka kutafuta suluhu la mgawanyiko ambao umeshuhudiwa kwa muda mrefu sasa.Aidha,suala la kilimo hasa cha miwa na mahindi pia litajadiliwa ili kuafikiana jinsi ya kuwasaidia wenyeji wanaotegemea kilimo kimaisha.Kwa sasa ibada ya wafu inaendelea.Marehemu Wamalwa alifariki miaka 15 iliopita akihudumu kama makamu wa rais wa rais mstaafu Mwai Kibaki.

Show More

Related Articles