HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaoishi Na Ulemavu Waombwa Kujiunga Pamoja.

Changamoto imetolewa kwa  wanaoishi na ulemavu kote nchini  kujiunga  vikundi  kama njia mojawapo ya kurahisisha  mawasiliano miongoni mwao  yanayohusiana na maswala ya uandikishwaji wao ili waweze kufaidika na miradi mbalimbali ya maendeleo kutoka kwa serikali.

Akizungumza  wakati  wakupeana   vifaa mbalimbali kwa  watu  33 wanaoishi na ulemavu kaunti ya Kwale  vilivyogharimu  jumla ya shilingi   nusu Milioni   Micky kiswili  afisaa kutoka bodi ya wadhamini ya   hazina ya kitaifa    ya  walemavu amesema kuwa bado asilimia kubwa ya watu  wa jamii hio  hawajasajiliwa  katika mpango huo wa serikali  hali anayoitaja kutokana na ukosefu wa ushirika miongoni mwao .

Show More

Related Articles