HabariMilele FmSwahili

Wanaharakati waandamana Nairobi kushinikiza serikali ya Uganda kumwachilia huru Bobi Wine

Mamia ya wanaharakati wanaandamana hapa jijini Nairobi wakati huu kushinikiza kuachiliwa huru mbunge ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki nchini Uganda Robert Kyagulanyi jina maarufu Bobi Wine. wanaharakati hao wakiongozwa na chama cha mawakili nchini wanaitihumu serikali ya Uganda kwa ukiukaji haki za binadamu kwa kumzuia mbunge huyo. Pia wameshutumu kuzuiliwa kwake katika gereza la kijeshi wakitaja kuwa kinyume na sheria. Bobi Wine anatarajiwa kufidishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda leo kujibu madai ya kumiliki silaha kinyume na sheria.

Show More

Related Articles