HabariPilipili FmPilipili FM News

Bungle La Kaunti Ya Kwale Yapinga Utafiti Wa Mdini Katika Kaunti Hiyo.

Bunge la  kaunti ya Kwale  linashikilia  kwamba   utafiti  wa  madini katika maeneo  mapya   unaolengwa kutekelezwa  na kampuni ya uchimbaji madini ya base titanium  hautafanyika hadi pale mwekezaji huyo atakapokubali kufidia waathiriwa  wa mradi huo kwa mjibu wa sheria,   kwani   wenyeji  huenda wakapoteza mashamba yao.

Wakizungumza na baadhi ya maskwota wa  Bwiti waliohamishwa kutoka eneo la Nguluku na Maumba huko  Lungalunga ili  kutoa nafasi kwa uchimbaji wa madini, kiongozi waliowengi  katika bunge la Kwale  Raia Mkungu  na mwakilishi wa wadi ya Ndavaya Juma Masudi Ngando wamesema hawataruhusu wakaazi kunyanyaswa  kwa kisingizio cha uchimbaji madini katika eneo zima la kusini mwa pwani  .

Hii ni kutokana na kile kinachodaiwa kuwa wenyeji walioamishwa kutoka Nguluku na Maumba  walilipwa fidia duni mno ya shilingi elfu 80  kwa ekari hali ambayo imewafanya wengi kuishi maisha ya uchochole

Show More

Related Articles