HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Rais Kenyatta aonya siasa zisiingizwe mwafaka wake na Raila

Rais Uhuru Kenyatta sasa amewaonya wakenya dhidi ya kuingiza siasa kwa ushirikiano kati yake na  kiongozi wa ODM Raila Odinga, akisema ushirikiano huo unalenga kuimarisha umoja na ufanisi wa taifa hili.

Akizungumza wakati wa hafla ya ukumbusho wa kifo cha babake ambaye ni rais mwanzilishi wa Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta, rais amesema maafikiano kati yake na Odinga hayakuwa ya mzaha tu bali yalikuwa na maana ya ndani ambayo kwa sasa wanajizatiti kuafikia.

Show More

Related Articles