HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Kunufaika Katika Maonyesho Ya Kilimo Ya Mwaka Huu Mombasa.

Maonyesho ya kilimo ya mwaka  huu yatakuwa na manufaa mengi  kwa vijana hasa katika sekta ya ubaharia na uhandisi wa baharini.

Hii ni kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya Bandari ya Mombasa Daniel Manduku, ambaye amewahakikishia wakenya kuwa bandari ya Mombasa, imewekeza kiwango cha kutosha cha fedha, kwenye maonyesho  ya Mombasa katika kutoa mafunzo hayo kwa vijana.

Akiwa kwenye zoezi la kukagua  matayarisho ya maonyesho ya kilimo Mkomani  hata hivyo Manduku  amekwepa kuzungumzia swala la ufisadi unaoizingira bandari ya Mombasa.

 

 

Show More

Related Articles