HabariPilipili FmPilipili FM News

Vita Dhidi Ya Ufisadi Vitaendelea, Asema Rais Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta ameendelea kushikilia kuwa vita dhidi ya ufisadi vitaendelea.

Akizungumza wakati wa ukumbusho wa miaka 40 tangu mwanzilishi wa taifa hayati mzee Jomo Kenyatta afariki rais Kenyatta  amewataka wakenya wote kushirikiana kumaliza zimwi hilo ambalo linaendelea kurudisha nyuma maendelea ya taifa.

Wakati huo huo rais Kenyatta amewakumbusha wakenya kuwa mwafaka wake na kinara wa upinzani Raila Odinga ni mwafaka wa manufaa kwa taifa na haupaswi kuingizwa siasa.

Naye naibu rais Willima Ruto amewahimiza wakenya kuendeleza umoja ambao hayati Jomo Kenyatta alikua akiuhimiza wakati wa uhai wake.

Wengine waliohudhuria hafla hio ni pamoja na kinara wa NASA Raila Odinga mamake rais Uhuru Kenyatta mama Margaret Kenyatta na wengineo.

 

Show More

Related Articles