HabariPilipili FmPilipili FM News

Mfanyibiashara Kumar Afikishwa Mahakamani Mombasa.

 

Mfanyibiashara Praful Kumar anaedaiwa kumhonga gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonko amefikishwa katika mahakama ya Mombasa akiwa anakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo kujaribu kumhonga Sonko shilingi milioni moja ili kuidhinisha ujenzi wa hoteli yake,kumshawishi kuendeleza ujenzi wa hoteli yake jijini Nairobi pamoja na kumhonga Sonko azuie ubomozi wa ghorofa zilizozidi.

Mfanyibiashara huyo hata hivyo amepinga mashataka yote matatu mbele ya jaji Henry Nyakweba.

Praful Kumar alitiwa mbaroni na maafisa wa kupambana na ufisadi nchini EACC Jumatatu usiku eneo la Kanamai kaunti ya Kilifi.

Kumar ataendelea kuzuiliwa hadi kesho ambapo uamuzi wa kuachiliwa  kwa dhamana au la utatolewa.

 

 

Show More

Related Articles