HabariMilele FmSwahili

LSK yamtaka rais Museveni kumuachilia huru Bobi wine

Chama cha mawakili nchini LSK kinamtaka rais wa Uganda Yoweri Museveni kumuachilia huru mwanasiasa Bobi Wine.Katika mkao wa pamoja na wanaharakati wa haki za kibinadamu hapa Nairobi, mwanachama wa LSK Charles Kanjama anazitaka serikali za afrika mashariki kumshurutisha Museveni kuheshimu haki za kibinadamu.Kanjama kadhalika anasema wataanda maandamano ya amani kesho hapa Nairobi kuelezea kutoridhishwa kwao na utawala wa Museveni.Kuzuiliwa kwa Bobi Wine kumezua ghadhabu za baadhi ya wenyeji wa Uganda wanaotaka kuachiliwa huru mbunge huyo.

Show More

Related Articles