HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakenya Watapata Cheti Cha Nidhamu Bila Malipo Katika Maonesho Ya kilimo Mombasa.

Kwa mara ya kwanza wakenya wataweza kujipatia cheti cha nidhamu kutoka kwa idara ya usalama papo hapo, wakati wa maoneshi ya kilimo ya Mombasa yanayotarajiwa kuanza tarehe 29 ya mwezi huu.

Mwenyekiti wa maonesho hayo Anisa Abdalla amewahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo ambayo huduma yake itakuwa bila malipo.

Anisa ameongeza kuwa katika maonyesho ya mwaka huu yatakuwa na faida zaidi hasa kwa vijana na kina mama.

Hadi kufikia sasa takribani waonyeshaji 180 tayari wamejisajili huku wengine zaidi wakitarajiwa kujisajili

Show More

Related Articles