HabariMilele FmSwahili

Kadhi mkuu amsuta Duale kwa kushutumu ushauri wake kuhusu maadhimisho ya Idd-ul Adha

Kadhi mkuu Ahmed Mudhar amepuuza shutuma dhidi yake kuhusiana na  maadhimisho ya siku kuu ya Idd ul-Adha iliyoandaliwa jana. Mudhar amesema hatatishwa katika kutekeleza majukumu yake. Hii ni baada ya baadhi ya viongozi wa kiislamu wakiongozwa na kiongozi wa wengi bunge Aden Duale kudai Mudhar alichangia migawanyiko miongoni mwa waislamu. Duale alimtaka Mudhar kukoma kutoa ushauri kuhusu siku ya maadhimisho hayo akidai hana haki kisheria kufanya hivyo.

Show More

Related Articles