Pilipili FmPilipili FM News

Kaunti Ya Kilifi Yaorodheshwa Nafasi Ya tatu Katika Maambukizi Ya Ugonjwa Wa Kudumaa Hapa Nchini.

Takwimu za ugonjwa wa kudumaa katika Kaunt ya kilifi  zinaendelea kupungua hii ni kulingana na Idara ya afya Kaunti hiyo.

Akizungumza eneo la Bamba wakati wa hafla ya  kusherekea mwezi wa kinamama kuwanyonyesha watoto wao, mratibu wa maswala ya lishe bora eneo hilo Ronald Ngunya anasema licha ya visa hivyo kupungua bado kilifi inashikilia nafasi ya tatu kote nchini huku Kaunti za Kitui na Pokot magharibi zikishikilia nafasi za kwanza na pili mtawalia.

Ameyataja  maeneo ya Kaloleni, Ganze na Magarini kama yalioathirika zaidi, huku takwimu zaidi zikionyesha kuwa asilimuia 26 ya watoto kote nchini wanaugua ugonjwa huo.

Naye  mratibu wa afya chini ya shirika la UNICEF katika Kauntu hiyo Jadin Ngolo amewataka kinamama kuwanyonyesha watoto wao kikamilifu kwa miezi sita mfululizo, bila kuwapa chakula chochote kama njia mojawapo ya kuboresha afya ya watoto sawia na kuwaepusha na ugonjwa huo.

Show More

Related Articles