HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mgomo baridi gereza la industrial area waingia siku ya pili

Mgomo baridi wa washukiwa wa uhalifu ambao wako rumande katika gereza la Industrial Area Nairobi umeingia siku yake ya pili hii leo ambapo wamesusia mlo na kuibua hali tete gerezani.

Wafungwa hao wamedai kunyanyaswa na maafisa wa polisi wa gereza hilo huku wakidai mmoja wao aliteswa hadi kufa huku mwengine ambaye ni mlemavu pia akijeruhiwa vibaya.

Juhudi za naibu kamishna wa magereza nchini za kutatua mzozo huo ziliambulia patupu huku washukiwa hao wakiitisha mkutano wa dharura na mkuu wa magereza nchini Isaiya Osugo la sivyo wataendelea kususia mlo.

Show More

Related Articles