HabariMilele FmSwahili

Mwanamke mmoja amuua mumewe kwa kumdunga na kisu Nyeri

Mwanamke mmoja wa umri wa makamo anazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Nyeri kwa madai ya kumuua mumewe kwa njia ya kumdunga kisu.Kulingana na kinara wa polisi Nyeri ya kati Kioko Muinde ni kuwa mwanamke huyo kwa jina Mukiri Mwiti alimdunga kisu siku ya alhamisi wiki jana alipofika nyumbani akiwa mlevi na akapelekwa hospitalini ambapo aliaga dunia hapo jana na hivyo kupelekea kukamatwa kwa mwanamke huyo.Inasemekana kuwa mwanamke huyo walikuwa wakizozana mara kwa mara na mmewe kwa jina Francis Mwiti aliyekuwa akiuza miraa katika eneo la Muthinga, eneo bunge la Tetu na wote walikuwa walevi kupindukia.Sasa mwanamke huyo atafunguliwa mashtaka ya mauaji.

Show More

Related Articles