HabariPilipili FmPilipili FM News

Waumini Wa Dini Ya kiisilama Washerehekea Siku Kuu Ya Eid-Ul-Adha.

Waumini wa dini ya kiisilamu wamehimizwa kudumisha amani  na umoja wakati huu  ambapo wanasherehekea siku kuu ya Eid-Ul-Adha.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya suala ya EID- iliyoandaliwa katika uwanja wa tononoka, katibu mkuu wa baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK SHEIK Mohamed KHALIFA, ametoa wito pia kwa wanaosherehekea kuwakumbuka masikini wakati huu wa sherehe.

Ameishukuru serikali kwa kuifanya siku hii ya mapumziko ili wakenya wote washerehekea pamoja.

Haya yanajiri wakati kukiwa na mgawanyiko kuhusu muonekano wa mwezi baadhi ya waumini wakitarajiwa kusherehekea Eid yao hapo kesho.

Show More

Related Articles