HabariPilipili FM News

Wakaazi Wa Kilifi Waombwa Kutochinja Wakati huu Wa Eid-Ul –Adha.

 

Waumini Katika  kaunti ya Kilifi watalazimika kusherehekea siku kuu  ya Eid-Ul –Adha bila kuchinja mnyama aina yoyote licha ya kuwa siku hii inajulikana kuwa ni sikukuu ya kuchinja.

Hii ni baada ya kuripotiwa mkurupuko wa maradhi aina ya RIFTVALLEY, miongoni mwa mifugo eneo hilo ambayo huenda ikadhuru afya ya binadamu.

Akidhibitsha hili katibu wa afya kaunti ya Kilifi daktari Anisa Omar amesema wanayama kama vile mbuzi na ng’ombe ndio walioathirika zaidi na maradhi haya.

Hata hivyo amesema licha ya kuwa maradhi hayo yameripotiwa kwa mara kwanza mwezi Juni mwaka huu,hakuna binadamu yoyote ambae ameathirika na maradhi hayo

Show More

Related Articles