HabariMilele FmSwahili

Serikali yatakiwa kutumia ripoti za TJRC kutanzua utata wa umiliki wa ardhi nchini

Serikali imetakiwa kutumia ripoti za tume ya ndugu kuhusu ardhi na ile ya maridhiano TJRC kutanzua utata wa umiliki wa ardhi nchini. Muungano wa mawakili tawi la humu nchini ICJ inasema mapendekezo hayo yatatoa mwelekeo kuhusiana na umiliki wa ardhi za msitu wa Mau na majengo yanayobomolewa hapa jijini.Mkurugenzi mkuu wa ICJ Samwel Muochi ameitaka serikali kusitisha mara moja ubomozi na ufurusho wa watu mau akidai ni kinyume na sheria.Muochi amesema ICJ iko tayari kuwasaidia wahanga wa shughuli hizi kusaka haki mahakamani.Kadhalika amemtaka mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin hajji kuwafungulia mashtaka maafisa wa serikali waliohusika katika uuzaji ardhi husika.

Show More

Related Articles