HabariMilele FmSwahili

Idara ya magereza yakanusha taarifa za mgomo baridi katika gereza la Industuial Area Nairobi

Idara ya magereza nchini imekanusha taarifa za kuwepo mgomo baridi katika gereza la Industrial Area Nairobi. Kamishna wa magereza Isiah Osugo ameiambia Milele fm taarifa zinazoenea kuhusiana na mgomo wa wafungwa ni porojo kwani shughuli za kawaida zinaendelea. Aidha anasema baadhi ya wafungwa wanaodai kudhulumiwa wanapinga uongozi wa msimamizi mpya wa gereza hilo

kauli ya Osugo inawadia baada ya kuibuka ukanda wa sauti wa mmoja wa wafungwa akielezea kutoridhishwa kwao na hali katika gereza hilo la Industrial Area. Gereza hilo lina jumla ya wafungwa 258.

Show More

Related Articles