HabariMilele FmSwahili

Swazuri amuandikia barua mkuu wa huduma za umma

Mwenyekiti wa tume ya ardhi Prof Mohamed Swazuri anayekabiliwa na shtaka la ufisadi, amemuandikia barua mkuu wa huduma za umma Francis Kinyua akipinga hatua ya wadhifa wake kukabidhiwa naibu wake kikaimu. Swazuri anasema bado yeye ni mwenyekiti wa tume hiyo na kwamba hatua ya naibu wake Abigael Mbagaya kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa muda imepotoka.Barua ya Swazuri inawadia huku mashirika ya kijamii yakitoa makataa ya siku 30 kwa makamishna wote wa NLC kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na tume hiyo kulaumiwa kwa biashara haramu za ardhi sawa na ubomozi unaoendeshwa nchini.

Show More

Related Articles