HabariPilipili FmPilipili FM News

Mashirika Ya Kijamii Yawataka Makamishna Katika Tume Ya Ardhi Kujiuzulu.

Kundi la mashirika ya kijamii sasa limewapa makamishna 9 wa tume ya ardhi nchini makataa ya siku 30 kujiuzulu.

Mashirika hayo yamewalaumu makamishna wa tume hiyo kwa utepetevu pamoja na kujihusisha na ufisadi.

Khelef Khalifa mmoja wa maafisa wa mashirika hayo anasema  wakenya hawana imani tena na tume hiyo ya ardhi..

Khalifa na wenzake wanasema makamishna hao wametumia nafasi zao kuwanyanyasa wakenya wanaotafuta huduma kuhusu matatizo ya ardhi huku wakiwapendelea baadhi ya wateja.

Show More

Related Articles