
Serikali ya kaunti ya Mombasa imeanza shughuli ya kubandika nyasi ya kubuni katika baadhi ya barabara za mji wa Mombasa, badala ya kupanda nyasi ya kiasili.
Hili limeubua mjadala kutoka kwa baadhi ya wenyeji wa mji huo, wengi wakitilia shaka mradi huo.
Ripota wetu wa masuala ya mazingira Dan Kaburu anaangazia suala hilo kwa kulinganisha nyasi hiyo ya kubuni na ile ya kiasili.