HabariMilele FmSwahili

Mwanamke mmoja ashambuliwa na fisi

Mwanamke mmoja wa umri wa miaka 25 anapigania uhai wake katika hospitali ya Machakos level 5 baada ya kushambuliwa na fisi katika barabara ya Nairobi Mombasa. Mwanamke huyo kwa jina Irene Mbithe, anasema alipewa lifti na lori moja ghafla dereva na abiria waliokuwa katika lori hiyo walitaka kumbaka na aliposita wakaamua kutupa nje  ya lori hilo.Ni baada ya tukio hilo alipataka na fisi aliyemla mkono wake mmoja na jicho.Polisi kutoka kituo cha Mtito Andei wanasema wameandikia barua shirika la wanyamapori kufidiwa msichana huyo

Show More

Related Articles